Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako na Naibu waziri Ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia walemavu, Stella Ikupa Alex ni miongoni mwa watu waliojitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Maria na Consolata.
Katika shughuli hiyo ya kutoa heshima ya mwisho, vilio na huzuni vilitawala huku mamia ya watu waliofika kuwaaga mapacha hao walioishi kwa miaka 21, na kugusa mioyo ya wengi wakishindwa kuzuia hisia zao za majonzi waliyonayo.
Mapacha Maria na Consolata wameagwa leo na wanatarajiwa kuzikwa leo baadaye kwenye makaburi ya masista yaliyopo Tosamaganga, mkoani Iringa.
Habari
Picha: Yaliyojiri katika ibada ya kuwaaga Maria na Consolata
By
|
- 1
Ibada hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu atayeshughulikia masuala ya Watu wenye ulemavu, Stella Ikupa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni