Jumamosi, 9 Juni 2018

KIMENUKA SALAH AKUTANA NA RAIS WA MISRI, AMUAMBIA ATAPAMBANA KAMA KAWA RUSSIA







Mshambuliaji nyota wa Misri, Mohamed Salah amesisitiza mbele wa Rais wa Misri, Abdel Fattah el Sisi kwamba atakuwa fiti kuitumikia nchi yake katika Kombe la Dunia.
Salah aliyasema hayo wakati Rais el Sisi alipowaalika Ikulu kwa ajili ya kuwaaga na kuzungumza nao kabla ya kwenda Russia.

Kulikuwa na hofu kubwa ya Salah mwenye umri wa miaka 25 kama angeenda Russia baada ya kuumia wakati akiitumikia Liverpool.


Salah aliumia baada ya kuangushwa na Sergio Ramos wakati wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kusababisha ateguge bega.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni