Ijumaa, 8 Juni 2018

Hali tete inayoendelea Libya inatupa wasiwasi:UN

Msichana huyu akichunugia dirishani akiwa Benghazi Libya ambako machafuko yamekumba sehemu mbali mbali.(Picha:UNSMIL/Maktaba)


Hali ya hatari dhidi ya raia kwenye mji wa Derna Mashariki mwa Libya inazusha wasiwasi mkubwa hasa kuhusu hatma ya raia, kufuatia mapigano yaliyoshika kasi na kundi la jeshi la jeshi la kitaifa nchini humo LNA kuarifu kudhibiti wilaya zilizo na idadi kubwa ya watu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya haki za binadamu mjini Geneva Uswis kuna madai kwamba raia wanashikiliwa kiholela huku wengine wakizuiwa kuondoka katika mji huo.
Hali ya kibinadamu inazidi kuzorota kukiwa na uhaba mkubwa wa chakula, maji na madawa na tangu Juni 5 hospitali pekee katika mji huo ulio na watu takribani 125,000 imefungwa na watu wanawake watatu wameripotiwa kufariki dunia kutokana na ukosefu wa hewa ya oxijeni waliyohitaji.
Msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Geneva ni Elizabeth Throssell
 (SAUTI YA ELIZABETH TROSSELL)
“Hofu yetu kwa raia na wapiganaji waliojisalimisha, kuweka chini silaha zao ni wagonjwa au waliojeruhiwa  au ambao hawashiriki mapigano, wote hao tuliorodhesha ukiukwaji mkubwa wa sheria za haki za binadamu na sheria za kimataifa za kibinadamu wakati wa mapigano kwa ajili ya kudhibiti eneo la Mashariki lenye mafuta na baadhi ya sehemu za mji wa Benghazi, visa vyote mwanzoni mwa 2017.”
Ameongeza kuwa wanazitaka pande zote katika mgogoro mjini Derna ikiwemo LNA na vikosi vya ulinzi vya Derna kuchukua hatua zote za kuwalinda raia, na pia kundi la LNA kuruhusu misaada ya kibinadamu kufika mjini humo bila pingamizi.
Pia ofisi ya haki za binadamu imezitaka pande zote kuhakikisha majeruhi na wagonjwa wote raia na wapiganaji wanapatiwa huduma inayohitajika ikiwemo matibabu na kuwezesha raia wanaotaka kuondoka salama mjini humo kufanya hivyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni