Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji amesema mwaka ujao wa
fedha, Tanzania itafanyiwa tathimini kuhusu deni la taifa.
Dk.
Kijaji ametoa kauli hiyo bungeni leo wakati akijibu swali la Mbunge wa
Mtambile, Masoud Abdalah Salim (CUF) ambaye alihoji ni lini deni la
taifa litafanyiwa uhakiki ili kuwe na hali nzuri ya uchumi.
“Mnaendelea kukopa na deni halifanyiwi uhakiki ni lini sasa mtafanya mkakati huu wa uhakiki kwa haraka,”amehoji.
Akijibu
swali hilo, Dk. Kijaji amesema Serikali haijawahi kuacha kulipa deni
hata mwezi mmoja ndiyo maana Tanzania bado inaaminiwa.
“Mikopo yote tunayokopa tunapeleka kwenye maendeleo ya kiuchumi na bado tunasisitiza kuwa deni letu ni himilivu.
“Kuhusu uhakiki wa deni letu katika mwaka ujao wa fedha itafanyiwa tathimini,”amesema.
Naye
Mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda amehoji ni lini Serikali
italeta sheria bungeni ya mikopo ili inapokopa wabunge wafahamu.
Akijibu
hilo, Dk. Kijaji amesema: ” Serikali tunapokopa tunafuata sheria na
katiba na imeendelea kusimamia deni la taifa kwa kuzingatia sheria ya
mikopo,”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni