Klabu ya Azam imemalizana na mshambuliaji wa Njombe Mji FC, Ditram Nchimbi kwa kuingia naye mkataba wa miaka miwili.
Nchimbi ameondoka Njombe Mji iliyoteremka daraja katika msimu uliomalizika hivi karibuni na sasa atakuwa sehemu ya kikosi cha Azam.
Usajili huo umefanyika ikiwa ni siku kadhaa baada ya Azam kumchukua aliyekuwa kocha wa Singida United, Hans van der Pluijm pamoja na mchezaji wake tegemeo, Tafadzwa Kutinyu.
Taarifa za ndani kutoka Azam zinaeleza kuwa bado harakati za usajili ndani ya klabu hiyo zinaendelea hivyo mashabiki wa timu hiyo watarajie mambo mazuri msimu ujao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni