Ijumaa, 8 Juni 2018

MAPYA YAIBUKA WARAKA WA KKKT: Waziri Mwigulu Nchemba,amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii

Image may contain: 2 people

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Merlin Komba, kupisha uchunguzi wa barua iliyoandikwa kwa maaskofu wa KKKT.

Waziri Mwigulu amesema, barua iliyosambaa katika siku za hivi karibuni haina baraka za serikali na wanafanya uchunguzi kujua chanzo na lengo la barua hiyo.

 Akizungumza leo Juni 8 katika mkutano na wanahabari, Dk Nchemba amesema taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii ni batili na siyo maelekezo ya serikali au wizara.

“Tunawaomba viongozi wa dini waendelee na kazi zao, nasema jamii iwe macho na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya jamii na wasifanyie kazi taarifa hizo,” amesema.

Kadhalika, Dk Nchemba amesema amefuatilia barua hizo na kuona zina mkanganyiko wa anuani.

“Viongozi wa dini wasiwe na taharuki na taarifa hizo, hazina baraka za Serikali. Wasisite kuwasiliana na Serikali kujua uhalali wake.” Amesema.

Pia Dk Nchemba amesema waraka wa viongozi wa dini uliotolewa miezi iliyopita ni jambo lililopita na hivyo akawataka viongozi wa dini waendelee na kazi zao.

Dk Nchemba amewataka viongozi wa dini kuendelea na kazi zao. “Nchi yetu ni moja na tunaishi kwa taratibu tulizojiwekea na tuna madhehebu mengi.” Amesema na kuongeza: “Wengine wameliona jambo hilo kama ajenda. Wananchi wawe makini, wasiwafuate watu hao wanaotaka kuwagawa.”


Mbali na hato Waziri Nchemba ameonya wanasiasa wanaoingilia jambo hilo kisiasa kwa kusema kwamba kama umakini usipowekwa amani ya nchi itavurugika na ingawa bado wanaendelea na uchunguzi kuwabaini wahusika ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni