
Klabu ya Yanga imebadili tarehe ya kufanya mkutano wake mkuu uliokuwa umepanwa kufanyika tarehe 17/06/2018, ambao sasa utafanyika tarehe 10/06/2018.
Taarifa iliyotolewa na kamati ya utendaji ya klabu hiyo leo imesema ukumbi utakaotumika kwaajili ya mkutano huo, utatangazwa baadaye.
Taarifa hiyo licha ya kutoweka wazi ajenda kuu za mkutano, imesisitiza kuwa mkutano huo utawahusu wanachama wenye kadi ambazo zimelipiwa (kadi hai) ambapo kadi mpya (za Posta) na zile za zamani zitatumika.
“Mwanachama lazima awepo kwenye register ya klabu yake,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni