Jumatano, 23 Mei 2018

KMC: ALIYEKUWA KOCHA WA MBAO FC, HATUFAI



 Uongozi wa Klabu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) iliyopanda daraja kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao wa 2018/19 umekanusha kuwa na mpango wa kumwania aliyekuwa kocha wa Mbao FC, Ettiene Ndayiragije (Pichani) .

Mwenyekiti wa KMC, Suzan Massawe amesema kocha huyo hana uwezo wala sifa za kuifundisha KMC kutokana na kuwa na rekodi isiyoridhisha kwenye ligi kuu akiwa na Mbao FC kiasi cha kulalamikiwa na mashabiki wake baada ya timu kuonesha dalili za kushuka daraja.

“Hatuwezi kuwa na kocha ambaye ametoka kufungwa mechi sita mfululizo, ingawa kufungwa siyo tatizo, lakini siyo kufungwa mechi sita mfululizo,” amesisitiza Suzan.

Kocha Ettiene raia wa Burundi, ndiye aliyewaibua wachezaji kadhaa wanaofanya vizuri kwenye Ligi Kuu msimu huu wakiwa na vilabu vingine, akiwemo Asante Kwasi na Jamal Mwambeleko ambao wako Simba, Salmin Hoza ambaye yuko Azam na Pius Buswita anayekipiga Yanga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni