Jumamosi, 26 Mei 2018

AzamFC imetangaza kumsajili Donald Ngoma

Baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe kuachwa na club yake ya Dar es Salaam Young Africans Donald Ngoma kwa madai ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu leo club ya Azam FC imetangaza good news kwa mashabiki wa Ngoma.
Azam FC leo wametangaza kumsajili Donald Ngoma ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa majeruhi ya muda mrefu, Azam wao wameonesha kuwa na imani na mchezaji huyo na kuamua kumpa mkataba.
Taarifa zinaripoti pia baada ya Azam FC kuingia mkataba na Donald Ngoma watampeleka Cape Town Afrika Kusini katika hospitali ya Vicent Pallot kwa ajili ya kumpima afya na kujua tatizo lake lililokuwa linamsumbua.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni