

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Rose Mdenye mwenye umri wa miaka 31 mkazi wa Swasa jijini Dodoma amedaiwa kuuawa na mumewe na kitu chenye nchi kali usiku wa kuamkia leo.
Jeshi la polisi jijini Dododma limedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa taarifa zaidi zitatolewa mara baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika.
Naye Kaimu mganga mfawidhi Hospitali ya Furaa Mkoa wa Dododma amedhibitisha kuupokea mwili wa marehemu Rose Mdenye majira ya saa 5 usiku ulipopelekwa na jeshi la polisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni