Jumamosi, 26 Mei 2018

BUNGE WAMLILIA BILAGO

Image may contain: 1 person, text





mbunge wa Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA), Kasugu Bilago anatarajiwa kuagwa Jumatatu ijayo bungeni mjini Dodoma.

Spika wa Bunge Job Ndugai ameomboleza kifo hicho akisema awali Mbunge huyo alilazwa katika Hospitali ya DCMC iliyoko eneo la Ntyuka Jijini Dodoma kwa matibabu.

Amesema Mwili wa Marehemu Bilago unatarajiwa kuagwa Bungeni Dodoma Jumatatu ijayo kabla ya kupelekwa Kakonko Mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi.

Taarifa za kifo cha Mbunge huyo zimethibitishwa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupitia kwa msemaji wake Aminiel Eligaeshi ambaye amesema walimpokea Bilago Jumanne wiki hii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni