
Baadhi yetu naimani wamewahi kufuga Mbwa na wengine
inawezekana wakawa hawawapendi kabisa Wanyama hawa ambao ni mojawapo ya rafiki
wazuri kwa binadamu.
Hapa tumeamua kukuandalia baadhi ya mambo muhimu ya kufahamu
kutoka kwa Mnyama huyu Mbwa naimani utaweza kujifunza zaidi sababu lengo letu
ni kukupa Elimu zaidi na zaidi.
1.Utafiti uliofanywa na baadhi ya
Wasomi kutoka chuo kikuu cha California walieleza kuwa, Mbwa huwa wanaona Wivu
hasa pale wanapoona mmiliki wake anaonesha mapenzi kwa kitu kingine au mtu
mwingine.
2. Unaambiwa pia Mbwa sio kwamba tu
wanaweza kuona katika rangi Nyeusi na Nyeupe (Black and White) lakini pia wanaweza kuona katika eneo lenye
rangi ya Bluu na Njano
3. Mara kadhaa umeona Mbwa wana
kawaida ya kuzunguka zunguka kwa haraka katika umbo la Duara na kisha kutulia,
unaambiwa sababu ya kufanya hivyo ni wanafurahia eneo ambalo lipo na wanafurahi
mazingira hayo
4. Mbwa wana misuli takribani 18 kwa
kila sikio.
5. Unaambiwa Marekani ndiyo nchi
yenye idadi kubwa ya Mbwa, inakadiriwa zaidi ya Milioni 75
7. Kuhusu suala la Kusikia, Mbwa
wana uwezo wa kusikia mara 4 zaidi ya Binadamu namna tunavyosikia.
9. Mbwa ana uwezo wa kunusa zaidi
1000 kwa 10 Milioni zaidi ya Binadamu
10. Mbwa wana uwezo mkubwa
wa kutambua Hisia za binadamu kama unaogopa, au una hasira mbwa wanaweza
kutambua vyema.
vyanzo:Buzzfeed.com pamoja na Picha kwa msaada wa Mtandao


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni