Jule Niles, mwenye umri wa miaka 38, anasema Ainsley, mwenye umri wa miaka 20, anakataa kumsaidia kupata nyumba ambayo ataweza kuishi na kujivunia kutokana na sasa kijana huyo kupata mafanikio.
“Fedha zimempanda kichwa chake, mimi ninalala kwenye baridi, wakati yeye ana ghorofa ya £ 700,000 ya kifahari na ndugu yake Cordi” -Jule Niles
Jule amesema alianza kuishi katika chumba kimoja miezi mitatu iliyopita baada ya uhusiano wake kuvunjika na mwanae Ainsley, mwenye umri wa miaka 20.
Aliongeza: “Ni chumba cha mabati kisicho na madirisha au kiti. Hakuna vyoo au maji ya kufanya usafi binafsi. Mwanangu Ainsley anapaswa kuangalia nyuma na kuangalia familia yake. Mimi ni mzazi na nastahili kutunzwa.” -Jule Nile
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni