
Rais wa Marekani Donald Trump
amefukuza kazi Waziri wa mambo ya nje, Rex Tillerson na kumteua mkuu wa
wa Shirika la Kijasusi, CIA, Mike Pompeo
Akimshukuru Bw Tillerson
kwa huduma yake kupita akaunti yake ya Twitter, Bw Trump amesema Waziri
mpya wa Mambo ya nje atafanya "kazi nzuri".Bw Tillerson, aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya mafuta ExxonMobil, aliteuliwa kwenye kazi hio mwaka jana.
Rais Trump pia alimpendekeza Gina Haspel kuwa mwanamke wa kwanza kuwa mkuu wa CIA.
Afisa wa juu katika Ikulu ya Marekani, amezungumza na BBC kuhusu muda wa tangazo hilo kutolewa: "Rais alitaka kuhakikisha kuwa timu yake mpya kabla ya mkutano na Korea Kaskazini na baadhi ya mikutano mengine ya kibiashara
Bw Tillerson alikuwa kwenye ziara rasmi ya Afrika wiki iliopita wakati ambapo alipata taarifa za ghafla za Trump kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Siku ya Jumamosi ,msemaji wake alisema amesitisha shughuli alizokuwa anapaswa kufanya nchini Kenya kutokana na hali yake ya kiafya kutokuwa nzuri

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni