Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May amesema jasusi wa zamani wa Urusi na binti yake walipewa sumu kali ambayo ni sehemu ya kundi la kemikali za sumu kwa jina Novichok.
Sergei Skripal na binti yake Yulia bado wanadaiwa kuwa mahututi hospitalini kufuatia jaribio hilo la kuwaua eneo la Salisbury Machi 4.
Kemikali hiyo ilitambuliwa na wataalamu katika maabara ya ulinzi na sayansi ya Porton Down.
Jina Novichok maana yake ni "mgeni" kwa lugha ya Kirusi na ziliundwa na Muungano wa Usovieti miaka ya 1970 na 1980.
Ni jina linalotumiwa kurejelea kemikali za sumu ambazo hushambulia mfumo wa neva mwilini.
Kutokana na taarifa hizo, Waziri mkuu May amesema Urusi imehusika kumshambulia Sergei Skripal.
Ni jina linalotumiwa kurejelea kemikali za sumu ambazo hushambulia mfumo wa neva mwilini.
Kutokana na taarifa hizo, Waziri mkuu May amesema Urusi imehusika kumshambulia Sergei Skripal.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni