Zaidi
ya watu milioni saba nchini Sudan kusini sawa na theluthi mbili ya watu
wote huenda wakakabiliwa na hali mbaya ya uhakika wa chakula katika
miezi michache ijayo kusipopatikana misaada ya kibinadamu.
Natts….
Haat Sudan Kusini mtoto Nyadane Kuony mwenye umri wa miaka minne akilia wakati anapimwa utapia mlo. Akiwa na babu na bibi yake walikimbia vita huko Bentiu 2016, baba yake alifariki dunia kabla hajazaliwa na mama yake kwa sasa hayupo. Binti huyo alianza matatizo ya utapia mlo vita vilipochachamaa .
Hivi sasa kukiwa na uhaba mkubwa wa chakula watu wamegeukia kula mianzi na matunda mwitu. Mine Pusk Luoch ana umri wa miaka 8 tu
Nimekuja hapa kula mianzi hii kwasababu hatuna chakula.”
Maelfu ya wakimbizi wa Sudan kusini wanaendelea kumiminika katika nchi jirani ikiwemo Kenya ambako kambi ya Kakuma inahifadhi zaidi wakimbizi 106,000 kutoka sudan kusini. WFP inawapa msaada wa chakula wanapopokelewa tu kama anavyofafanua Martin Karimi msemaji wa shirika hilo nchini Kenya.
“Tunapokea takribani watu elfu moja kila mwezi, wanapowasili WFP inawapa mlo wa moto kabla hawajapewa vipande vya ardhi ambako wataendelea kupokea mgao wa chakula pamoja na fedha taslim kutoka WFP.”
Hivi sasa WFP inatoa chondechonde kwa wahisani na wafadhili kutoa fedha ili kusaidia shirika hilo kuokoa maisha ya maelfu ya wakimbizi hao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni