Jumanne, 13 Machi 2018

AJALI YA GARI YANYANG'ANYA MAISHA YA WATU 38 ETHIOPIA:

Image may contain: one or more people and outdoor

 Ajali hiyo ya basi (lililoporomoka kutoka mlimani) imetokea kwenye wilaya ya Legambo iliyopo kwenye mkoa wa Amhara kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Addis Ababa.

Vyombo vya usalama vya nchi hiyo vimethibitisha kuwa wanaume 28 na wanawake 10 wamekufa kwenye ajali hiyo.

Wengi wa waliofariki ni wanafunzi wa vyuo vikuu nchini humo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni