
Uongozi wa FIFA umeitoza faini klabu ya Besiktas ya Uturuki baada ya paka kuingia ndani ya Uwanja wakati wa pambano dhidi ya Bayern Munich.
Faini hiyo imekuja mara baada ya Paka kuingia Uwanjani wakati Besiktas ilipoikaribisha Bayern Munich kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.
Kitendo cha Paka kuingia Uwanjani kilisababisha Mwamuzi wa mchezo huo kusimamisha mpira kwa muda na kuanza harakati za kumtoa nje ya Dimba.
FIFA wameeleza kuwa kutokea kwa tukio hilo ni maandalizi mabovu ya uongozi wa Besiktas kushindwa kujipanga vizuri kuelekea mechi hiyo mpaka Paka huyo kuleta usumbufu Uwanjani.
Mechi hiyo ilimalizika kwa Bayern kushinda mabao 3-1 na kuifanya Bayern ifuzu hatua ya robo fainali kwa jumla ya mabao 8-1, kufuatia ushindi wa mabao 5-0 kwenye mchezo wa kwanza huko Ujerumani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni