Jumatano, 7 Machi 2018

MATESO YA KUKOSA MAJI WILAYANI MALINYI MKOANI MOROGORO



Zaidi ya miaka 40 wananchi wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro hawajawahi kuyaona maji yakitoka kwenye bomba hivyo wameiomba serikali kuhakikisha inawapatia huduma hiyo muhimu kwani wamekuwa wakipata magonjwa ya mara kwa mara ikiwemo homa za matumbo.
Wananchi hao wamesema tangu mwaka 1974 walipotumia maji kwa mara ya mwisho kwa sasa wanatumia maji ya visima na mtoni ambapo kipindi cha kiangazi maji hukauka kwenye visima huku wakati wa masika maji ya visima huchafuka kwa maji machafu kuingia ndani ya visima hivyo.
Hata hivyo wakati wananchi hao wakitoa vilio vyao hivyo, Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amewasili wilayani Malinyi kushuhudia maendeleo ya mradi mkubwa wa maji unaotarajiwa kumaliza tatizo hilo la muda mrefu kwa wakazi hao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni