Leo March 16, 2018
Mwanaume mmoja Raia wa Denmark ambae alikutwa na viungo vya sehemu za
siri za wanawake akiwa ameviweka kwenye freezer amehukumiwa vifungo
viwili vya maisha na Mahakama ya Afrika Kusini.
Mwanaume
huyu Peter Frederiksen amehukumiwa kwa makosa ya kumbaka mtoto na kuua
mke wake, ambapo madai ya kukutwa na viungo vya sehemu za siri za
wanawake yalitupiliwa mbali na mahakama baada ya kukosa ushahidi wa
kutosha.
Frederiksen amehukumiwa kwa mashtaka 36
ambayo alishtakiwa nayo mwaka jana 2017 ikiwa ni
pamoja na kuandaa video za ponografia zinazohusisha watoto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni