Jumamosi, 3 Machi 2018

Afungwa Jela kwa kosa la kumchezea rafu Rais Uwanjani

Leo March 3, 2018 Stori nayokusogezea ni kuwahusu Watu wawili ambao wamefungwa jela baada ya kumchezea vibaya Rais Pierre Nkurunziza katika mchezo wa mpira wa miguu uliomshirikisha Rais huyo wa Burundi.
Rais Nkurunziza ambaye pia ni anasali katika Kanisa la Evangelical Christian hupenda kusafiri na Timu yake ya mpira wa miguu ya Haleluya FC pamoja na Kwaya  iitwayo “Komeza Gusenga”
Timu ya Rais Nkurunziza ilikuwa ikicheza na timu nyingine kutoka Kaskazini mwa nchi hiyo katika Mji wa Kiremba.

Katika mchezo huo uliowajumuisha wakimbizi wa kutoka Congo ambao hawakufahamu kama Rais Nkurunziza pia ni miongoni mwa mchezaji ambao hao ndio walimchezea rafu.
Mara nyingi Rais Nkurunziza anapocheza katika michezo ya kirafiki wapinzani wake humpatia nafasi ya upendeleo na kumuache atawale na hata kufunga magoli lakini katika mchezo huo haikuwa hivyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni