Leo March 3, 2018 nikuambie tu Tanzania
imebarikiwa kuwa na madini ya aina mbalimbali ikiwemo Tanzanite ambayo
hayapatikani nchi nyingine yoyote duniani.
Hata hivyo, Mgunduzi wa madini hayo ya Tanzanite Mzee Jumanne Ngoma amesema kuwa licha ya kugundua madini hayo miaka 52 iliyopita bado hakuna alichonufaika nacho.
Mzee Ngoma amesema kuwa anatamani kuonana na Rais John Magufuli
ili amueleze adha anayokutana nayo kwa sababu anaumia kuona hathaminiwi
wala kunufaika na chochote licha ya ugunduzi alioufanya.
“Nina mengi ya kumwambia Rais Magufuli kuhusu madini yaliyopo Tanzania mengine ni siri ya nchi siwezi kuyaweka hadharani,” -Mzee Ngoma
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni