Jumanne, 27 Februari 2018

RAMAPHOSA AFANYA MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI

Image may contain: 2 people, people sitting



Rais mpya wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amefanya mabadiliko "muhimu" kwenye baraza la mawaziri ikiwa ni uamuzi wa kwanza mkubwa kuufanya tangu kutwaa madaraka hayo.
Ramaphosa amemrudisha kwenye uwaziri wa fedha, Nhlanhla Nene (aliyeondolewa kwenye nafasi hiyo na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Jacob Zuma), pia amemteua David Mabuza kuwa makamu wa rais (Mabuza ni makamu mwenyekiti wa ANC) na amemteua aliyekuwa mpinzani wake kwenye kuwania uenyekiti wa ANC, Nkosazana Dlamini-Zuma kuwa waziri kwenye ofisi ya rais.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni