Kutoka nchini Marekani katika Jimbo la
Florida zaidi ya watu 17 wanaripotiwa kufariki dunia, 15 wakiwa
wanafunzi na wengine kujeruhiwa baada ya shambulio la risasi
lililofanyika katika eneo la shule ya Marjory Stoneman Douglas High
School iliyopo Parkland lililofanywa na kijana wa miaka 19 jana February
14, 2018.
Kijana huyo aliyetambuliwa kwa jina la Nikolas Cruz alikuwa ni mwanafunzi katika shule hiyo lakini inaelezwa kuwa alifukuzwa. Alitumia silaha aina ya AR-15-riffle, magazine, pamoja na mabomu ya mkono kutekeleza tukio hilo.
Maaskari wa eneo hilo wameeleza kuwa kabla ya kuanza kushambulia katika eneo hilo, Nikolas aliwasha kengele ya tahadhari ya moto ili kufanya wanafunzi watoke nje na walivyotoka akaanza mashambulizi.
Kijana huyu alifukuzwa shule kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu na tayari amekwisha kamatwa na mahojiano yanaendelea.
Inaripotiwa kuwa eneo hilo limejaa watu, familia mbalimbali za watoto wanaosoma shule hiyo zimefurika kufahamu usalama wa watoto wao na kuwachukua na kutambua miili iliyokufa kama ni ya watoto wao.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni