Alhamisi, 15 Februari 2018

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ ala kiapo leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt John Pombe Magufuli amemuapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed ambaye anachukua nafasi ya Luteni Jenerali, James Mwakibolwa ambaye amestaafu.

Luteni Jenerali Mohamed aliteuliwa Februari 14, 2018 na Rais Magufuli kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ na kupandishwa cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali.
Hata hivyo katika uteuzi huo Rais Magufuli aliwapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali J.G. Kingu, M.S. Busungu, R.R. Mrangira, B.K. Masanja, G.T. Msongole, A.F. Kapinga, K.P. Njelekela, A.S. Bahati, M.E. Mkingule na S.S. Makona.
Mabrigedia jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi baadaye taarifa ya Ikulu imeeleza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni