mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Jumatatu, 22 Januari 2018
WHO yajipanga kuleta mabadiliko katika sekta ya Afya mwaka huu
Mkurugenzi wa shirika la Afya ulimwenguni WHO Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus amehutubia bodi ya shirika hilo hilo hi leo mjini Geneva katika hafla ya ufumbuzi wa kikao cha 142 cha bodi ya uongozi wa WHO .
Katika hutuba yake bwana Tredros amepongeza juhudi la shirika la WHO , chini ya uongozi wa kuleta mabadiliko ya usawa wa kijinsia katika viwango vya uongozi wa WHO, kwa kuwa amini wanawake katika nafasi muhimu na nyeti jambo ambalo ni hitoria katika uongozi wa shirika hilo.
Bwna Tedros amepongeza pia jitihada za WHO kuleta hamasa na mabadiko katika serikali za nchi nyingi uilimwenguni, asasi za kiraia na mashirika ya kibindamu katika swala la huduma ya afya kwa wote akisema.
“Tumeanza mchakato mpya wa kujumuika pamoja na mashirika ya kiraia ili kuongeza sauti zetu za pamoja ambazo ni nguvu zaidi kuliko ile iliyogawanyika. Na tumekamilisha mwaka sasa kuhusu makubaliano ya Tokyo kuhusu huduma ya afya kwa wote ambako tulishuhudia ahadi isiyokuwa ya kawaida kwa vyongozi wa kisiasa katika kuunga mkono maono yetu ya afya kwa wote”
Na kuhusu jitahada za WHO kutokomeza magonjwa yasio ambukizwa Dr. Tedros alisema…
“Kwa kasi kubwa Tumeanzisha Tume ya ngazi ya Juu itakayotuwezesha kukabiliana na magonjwa yasiyoambukizwa na pia TB, ambayo yote yamepewa nafasi ya juu kushughuikiwa katika katika mkutano mkuu wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa baadaye mwaka huu”
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni