Nyota wa zamani wa kandanda duniani
George Opong Weah ameapishwa kuwa rais wa Liberia katika sherehe
iliyohudhuriwa na maelfu ya watu katika mji mkuu Monrovia.
Weah
amechukua nafasi ya rais wa kwanza mwanamke kuwahi kuchaguliwa kuongoza
taifa la Afrika Ellen Johnson Sirleaf, ambaye amestaafu.Kuingia kwa Weah madarakani kunakamilisha shughuli ya kwanza ya amani ya mpito nchini humo tangu mwaka 1944.
Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi wa mataifa kadha pamoja na nyota wa kandanda duniani.
Akihutubu baada ya kula kiapo, Bw Weah amesema: "Nimekuwa katika viwanja vingi maishani, lakini sijawahi kuhisi hivi."
Leo January 22, 2018
nyota wa zamani wa soka Duniani George Weah ameapishwa kuwa Rais wa
Liberia katika sherehe iliyohudhuriwa na maelfu ya watu katika mji mkuu
wa nchi hiyo Monrovia.
Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi
wa mataifa kadha pamoja na Mastaa wa soka duniani. Akihutubia baada ya
kula kiapo, Weah amesema: “Nimekuwa katika viwanja vingi maishani, lakini sijawahi kuhisi hivi.”“Nitafanya zaidi ya mchango ninaotarajiwa kutoa ili kutimiza matarajio yenu, lakini naomba nanyi mtimize matarajio yangu, siwezi kutimiza haya peke yangu.”– George Weah
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni