Jumamosi, 20 Januari 2018

Waziri Mkuu ameamuru kukamatwa na kuhojiwa Kigogo wa MUWASA kwa tuhuma hizi



January 20, 2018 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameiamuru Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  Mkoa wa Mara kumkamata na kumhoji Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Musoma (MUWASA) Eng. Gantala Said kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi ya maji Bunda.
Ameagiza pia TAKUKURU imhoji Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Nyakirang’anyi Muhuza Mumay ambaye ndiye Mkandarasi anayejenga mradi huo unaotoa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda eneo la Nyabehu hadi Bunda Mjini.
Waziri Mkuu ameeleza kuwa amefikia uamuzi huo baada ya Mkurugenzi huyo  kushindwa kueleza sababu zilizosabisha mradi huo wa Bunda kutokamilika japokuwa serikali imetoa pesa nyingi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni