Waziri wa Mambo ya Ndani, Dr. Mwigulu Nchemba leo January 20, 2018 amelitaka Jeshi la Polisi nchini kutafuta namna ya kupunguza wahalifu wanaokamatwa kwa makosa kama uzururaji ili kupunguza mrundikano kwenye mahabusu.
Ameeleza
kuwa suala hili pia litaepusha watuhumiwa wanaopelekwa mahabusu kwa
makosa ya uzururaji kupata nafasi ya kuzungumzia masuala ya uhalifu na
watuhumiwa waliozoea.
Kwa
upande mwingine Dr. Mwigulu ameagiza wananchi kushirikiana na serikali
katika ujenzi wa vituo vya polisi kwa kuwa suala la ulinzi ni ajenda ya
kila Mtanzania na linapaswa kupewa kipaumbele.
Akizungumza
na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Dr. Mwigulu amesema
kuwa mkakati wa Halmashauri hiyo kujenga kituo cha kisasa cha polisi ni
kitendo cha kupongezwa kwani wanalenga kukomesha uhalifu wa aina zote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni