Naibu
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar,
Salum Mwalimu amefanikiwa kurudisha fomu ya kugombea Ubunge jimbo la
Kinondoni huku akiwataka wanachama wa chama hicho kuwa wavumilivu katika
kipindi hiki cha muda mfupi.
Mhe.
Salum ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na baadhi ya vyombo vya
habari vilivyoweza kujitokeza katika ofisi za Tume ya Uchaguzi Manispaa
ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo alasiri(Jumamosi).
"Nimefarijika
kwamba fomu imepokelewa na haina mapungufu yeyote yale, kwa hiyo hatuna
shaka lolote katika fomu yetu kwa maana tumeikagua na kuuliza maswali
katika kipengele jinsi tulivyojaza na wakatujibu tupo sahihi. Imani
yangu ni kwamba hawajaona kosa ambalo wanaweza kulikalia kimya
walisubiri ili lilete matatizo baadae", alisema Mhe. Salum Mwalimu.
Aidha,
Mhe. Salum aliendelea kufafanua baadhi ya mambo kwa kusema hatoweza
kutangaza siku ya kuanza kampeni rasmi mpaka itakapofika alasiri ya
kesho (Jumapili) kwa maana muda huu wa katikati ameuacha ili kama
kutakuwa na watu waweze kuweka mapingamizi yao.
"Kwa
hiyo baada ya muda huo kupita siku ya kesho bila ya shaka nitakuwa
mgombea rasmi wa jimbo la Kinondoni ambaye nisiyekuwa na doa kwa ajili
ya mapambano hayo", alisistiza Mhe. Salum Mwalimu.
Pamoja
na hayo, Mhe. Salum aliendelea kwa kusema "kikubwa labda niwaambie
hatukuja ku-beep wala hatu-beep kamwe haitakuja kutokea ku-beep katika
jimbo la Kinondoni. Tunamaanisha na tunaamini kabisa kama nidhamu ya
siasa waliyoikataa, hapa watairudisha na wasipoikubali kuirudisha
Kinondoni maana yake ustaarabu katika siasa tunaamini utakuwa
umekwishamalizika. Hatutokuwa wa kulia, safarii hii ikibidi
tutawasababisha wale waliosababisha sisi tunalialia wao ndio walie".
Kwa
upande mwingine Mhe. Salum Mwalimu amesema amedhamilia na amejitoa
kusimamia haki ya wananchi wa Jimbo la Kinondoni na kuahidi hatoweza
kuyumba katika hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni