Alhamisi, 25 Januari 2018

Usijifanye jini kujua, wakati una silaha za nguvu za giza”-Ruby

Muimbaji wa Bongofleva Ruby bado watu wanasubiri kwa hamu ujio wake mpyaa baada ya kukaa kimya bila kutoa ngoma toka mwezi April 2017, kimya cha Ruby wengi hawakifurahi kutokana na wao kuamini kuwa Ruby ana uwezo mkubwa.
Mashabiki wengi kwa sasa wanasubir ujio mwingine wa Ruby lakini leo muimbaji huyo ametoa ya moyoni mwake kupitia ukurasa wake wa instagram kwa kuandika ujumbe huu, licha ya kuwa hajamtaja moja kwa moja ni ujumbe ambao ana mlenga nani na amekusudia nini.

“Kunawatu ni wapuuzi ili ww mwerevu utoboe lakin usimdharau yule mpuuzi bila upuuzi wake ww usingeonekana mwerevu kazi ya Mungu muachie Mungu….usijifanye jini kujua sana wakati unasilaa za maangamizi ya nguvu za giza umezikalia watazama kibanzi ndani ya jicho la mwenzako wakati ww una boriti ndani yako je utaitoaje…!”
“Watanzania tumepewa kilakitu cha kutufanya tuwe matajiri lakin tatizo wengiwetu vidole vyetu virefu sana kukosoa tunamidomo sana mpaka kunamda unatamani usingekuwa mtz but unaacha kusudi la Mungu litimie tu 🤷🏼‍♀️😊truth hurts but change 🇹🇿❤️🙏🏽najitahidi kupapenda nilipo but God help me 🙌🏽🤴💪🏾#one bullet a thousands people”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni