Ijumaa, 19 Januari 2018

TUYATUNZE MAZINGIRA


 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wanaoishi kwenye mipaka kati ya Buguruni Mivinjeni na Sharifu Shamba pamoja na Mtoni kwa Azizi Ali kuwa watunzaji wazuri wa mitaro ya maji kwani ni mali yao wenyewe ila serikali iko kutekeleza.
Makamu wa rais aliyasema hayo wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku mbili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kuta za bahari na mitaro ya maji jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais aliwaeleza wananchi hao kuwa mabadiliko ya tabia nchi yameathiri shughuli za kiuchumi , kijamii na kimazingira na hivyo kuwataka kila mmoja kujishughulisha katika suala la kusafisha na kuhifadhi mazingira .
“Ubaya wa mazingira ukiyaharibu yanakuadhibu.” alisisitiza makamu wa Rais








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni