
Selvarani Kanagarasu, mfanyikazi
anayetegemea mshahara wa siku kutoka jimbo la kusini nchini India la
Tamil Nadu amekataa kuolewa na badala yake akaamua kumiliki ng'ombe wa
mchezo wa kupigana kwamafahali kulingana na mwandishi wa BBC Tamil
Pramilan Krishna.
Bi Kanagarasu mwenye umri wa miaka 48 alikuwa
kijana wakati alipoamua kwamba alitaka kufuata nyayo za babake na babu
yake ambao walifuga ng'ombe wa kiume walioshindana katika mchezo ya
jimbo hilo ya kupigana kwa mafahali kwa jina Jallikatu.Jallikatu ni mchezo maarufu kwa karne kadhaa jimboni Tamil Nadu na huchezwa wakati wa msimu wa kuvuna wa Pongal mwezi Januari.
Maelfu ya watu hufukuza ng'ombe ili kuchukua zawadi zilizowekwa katika pembe zao.
Mchezo huo haukichezwa kwa kipindi cha miaka miwili kufuatia marufuku ya mahakama ya juu kwa madai kwamba walikuwa wakiwafanyia wanyama hao ukatili.
Lakini kufuatia maandamano katika jimbo hilo, serikali ya jimbo hilo iliamua kuruhusu kuendeleaa mnamo mwezi Januari 2017 na hivyobasi kupuuzilia mbali marufuku iliowekwa.
''Babangu na babu yangu walifuga ngombe na kuwachukulia kama watoto wao'', alisema.
Jukumu la kuendeleza utamaduni wa kifamilia lingemwangukia nduguze bi Kanagarasu, lakini anasema hawakuwa na muda wa kuwaangalia wanyama hao.
Hivyobasi akaamua kuchukua jukumu hilo.
Ng'ombe anayemfuga ,kwa jina Ramu ni mnyama mwenye umri wa miaka 18 ambaye ni lejendari katika eneo hilo.
Ramu ameshinda mashindano matano kati ya saba ya Jallikattu ambayo alishiriki, akishinda zawadi kama vile sare na sarafu ya dhahabu kwa mmiliki wake.
''Ramu ni mwanangu wa kiume .Alishinda zawadi lakini cha muhimu alinishindia heshima katika kijiji chetu'', alisema akiongezea kuwa Ramu ana upendo mwingi licha ya kimo chake na hasira katika mashindano ya Jalikattu.
Kwa miaka mingi, watu wengi wamejeruhiwa ama hata kuuawa katika mashindano hayo.
Mamia wakiwemo mashabiki wameuawa ama hata kujeruhiwa .
Alimnunua wakati alipokuwa umri wa miaka 10.
Mmiliki wake alitaka kulipwa fedha nyingi lakini baadaye akakubali kumuuzia Ramu kwa kiwango cha chini baada ya kumwambia kwamba alitaka kumfuga ng'ombe huyo lakini hana kiwango cha fedha anachotaka

Uamuzi wa bi Kanagarasu wa kumwangalia ng'ombe huyo badala ya kuolewa sio wa kawaida hususan katika maeneo ya mamshambani nchini India.
Anasema nduguze na watu wa familia yake walishangazwa na hatua hiyo lakini baadaye wakaikubali.
Na ukakamavu wake umemfanya aheshimiwe na familia yake na wanakijiji wengine, huku akiendelea kumfuga ng'ombe huyo anayempatia kipato cha kutosha .
Nyumba yake ndogo ina jiko na chumba kimoja cha kulalia, ambacho pia ndio sebule na eneo, la kulalia.
Yeye hupata kipato cha Rupee 200 ambazo ni sawa na dola 3.15 kwa siku na anatumia fedha zote kuhakikisha kuwa Ramu yuko katika hali nzuri.
Mbali na nyasi na matawi ya mchele wanayopewa ng'ombe wengi katika jimbo la Tamil Nadu , pia anakula nazi, tende, ndizi njugu, mtama na mchele.
'Kulikuwa na siku ambapo nilikula mara moja kwa siku ili niweze kuweka fedha za kumnunulia Ramu chakula'', anasema.Mbali na chakula chake maalum, Ramu uhitaji mazoezi ya kila mara.
Hivyobasi bi Kanagarasu humchukua kila siku katika kidimbwi cha maji kilichopo kijijini ili aweze kuogelea kwa lengo la kuimarisha magoti yake.
''Binamu yangu Rajkumur pia humtembeza na kumfunza kukabiliana na wapinzani wake katika mchezo wa Jalikattu''.
''Pia hupata ripoti ya hali ya afya ya Ramu kutoka kwa daktari wa wanyama kabla ya kila shindano la Jalikattu ili kuhakikisha kuwa Ramu anafuzu'', anasema

Kutokana na ufanisi wa Ramu katika mashindano ya Jalikattu, watu wengi wametaka kumnunua ng'ombe huyo.
Mmoja wa ndugu zake Indira Selvaraj anasema alikataa ombi la hadi Rupee 100,000 kumuuza Ramu.
Anataka kumfuga ng'ombe huyo,kumuandaa kwa mashindano ya Jalikattu ndio lengo kuu la maisha yake.
Tulishindwa kumshawishi kukubali ombi letu. Sasa tumekubali kwamba hakuna gharama ya kufuta malengo ya mtu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni