Kikosi cha timu ya Simba kimewasili katika uwanja wa ndege wa Bukoba
asubuhi ya leo tayari kwa maandalizi ya mchezo wao wa Jumatatu Januari
22, mwaka huu dhidi ya wenyeji wao Kagera Sugar, mchezo utakaopigwa
katika dimba la Kaitaba na
Simba ambayo jana ilishinda mchezo wake wa raundi ya 13 kwa mabao 4-0
dhidi ya Singida United kwenye uwanja wa Uhuru, inakwenda kukutana na
Kagera Sugar ambayo ilikwamisha mipango yake ya ubingwa msimu uliopita.
Kagera Sugar ilitibua mipango hiyo April 2 mwaka jana baada ya kuifunga
Simba mabao 2-1 kwenye mechi iliyopigwa uwanja wa Kaitaba hivyo kuinyima
nafasi ya kurejea kileleni ikibaki na alama 55 katika nafasi ya pili na
kuwaacha Yanga wakiwa na alama 56 kileleni.
Endapo Simba ingeshinda mchezo huo ingefikisha alama 58 hivyo huenda
ingetwaa ubingwa kutokana na bingwa wa msimu uliopita kupatikana kwa
tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, baada ya timu hizo mbili za
Kariakoo kufungana pointi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni