Ijumaa, 19 Januari 2018

KUKOSEKANA KWA DHAMANA:


Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi 'Sugu' amerudishwa rumande hadi Jumatatu ijayo ambapo kesi yake ya kutoa matamshi ya uchochezi itaanza kusikilizwa mfululizo.




Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini CHADEMA, Joseph Mbilinyi 'Sugu' amerudishwa rumande hadi Jumatatu ijayo baada ya kukosa dhamana kufuatia Kesi inayomkabili ya kutoa matamshi ya uchochezi itakayoanza kusikilizwa mfululizo.
Hakimu Mkazi Mfadhiwi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, amesema sababu ya mbunge huyo na mwenzake, Emmanuel Masonga kunyimwa dhamana ni hofu ya huenda wasihudhurie mahakamani hapo mara kwa mara watakapohitajika.




 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni