Ijumaa, 26 Januari 2018

Taarifa rasmi kuhusu afya ya Mzee Majuto



Afya ya msanii wa filamu, Amri Athuman aka Mzee Majuto inaendelea kuimarika daada ya siku ya jana (Januari 25) kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii Afisa Habari wa Chama Cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni, Jafari Makatu amesema baada ya jana muigizaji huyo kufikishwa hospitali ya Muhimbili na kuangaliwa na daktari, alipewa kitanda cha kupumzika na baadaye kuruhusiwa.
“Ni kweli alipelekwa Muhimbili lakini hakulazwa kama baadhi ya watu walivyoripoti, alipewa kitanda kwaajili ya kupumzika na kusubiria vipimo na baada ya kufanyiwa vipimo aliruhusiwa kurudi nyumbani na akaambiwa leo aende tena kwaajili ya vipimo zaidi,” alisema Jafari.
Mapema mwaka jana muigizaji huyo mkongwe alitangaza kustaafu kuigiza na kudai kwa sasa amefungua kampuni yake ya masuala ya filamu.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni