Mwendesha Pikipiki kutoka Uarabuni
ameamua kuizunguka Afrika nzima anakusudia kufanya ziara yake katika
nchi 47, akianzia safari yake nchini Oman.
Maher Al Baruan
amepania kuweka historia ya kuwa raia wa kwanza wa Oman kuizunguka
Afrika akitokea kwenda kusini kupitia mashariki kisha atapanda Oman
kupitia Magharibi mwa Afrika.Safari yake ilianzia nchini Oman mnamo mwezi wa saba mwaka 2017.
Mpaka sasa amekwisha safiri kwa miezi 7 na anasema safari yake itachukua zaidi ya mwaka kuikamilisha.
Wahenga wanasema, msafiri kafiri na mwenda pole hajikwai.
Lakini je, amejifunza nini katika safari yake? Akiwa mjini Bujumbura Maher Al Baruan ameelezea mambo matatu ambayo amejifunza kuhusu Afrika.
Usalama ni jambo muhimu katika safari yoyote.
Changomoto kubwa Maher Al Baruan anasema anajihisi yuko katika hali ya hatari anaposafiri kwa sababu hajui atakutana na nani.
Anasema hata wanyama pori huwa ni jambo la kujitahadharisha.
Hata hivyo, anaelezea kuwa hajawahi kupata kisa chochote cha kumdhuru
Maher Al Baruan amegundua kwamba waendesha pikipiki wengi ambao amewaona hawatilii maanani sheria za barabarani na hasa za usalama kwa kuvaa kofia ngumu.
'Ningewashauri waendesha pikipiki wafuate sheria za barabarani, wasivue kofia ngumu kwa sababu hizi zote ni kwa ajili ya usalama wao' ameelezea Maher Al Baruan.
Maher anasema kuwa katika safari yake anakaa siku 35 kwa kila nchi anayoifikia ili kufahamu zaidi namna ambavyo watu wanavyoishi katika nchi hizo pamoja na kujua tamadani na kupata vionjo vya chakula.
Maher anataka kurudisha zama za babu zake wa Oman waliokuwa wakisafiri kanda ya Afrika Mashariki.
"Kila mmoja akishajua kwamba natoka Oman, wanaipenda nchi ya Oman na wanaiheshimu," anaelezea Maher Al Baruan
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni