Ijumaa, 26 Januari 2018

Dunia kushuhudia pambano kali Wilder dhidi ya Ortiz

Bondia, Deontay Wilder yupo katika mazoezi mazito kwaajili ya mpambano wake dhidi ya Luis Ortiz unatarajiwa kufanyika machi 3 mwaka huu.

Wilder ataingia ulingoni kutetea mkanda wake wa WBC uzito wa juu dhidi ya Mcuba asiyepigika,Luis Ortiz huko Barclays Center, Brooklyn.

Na endapo atafanikiwa kuurudisha mkanda huo atakuwa sehemu ya watu watakao hudhuria pambano kubwa na la kihistoria kati ya  Anthony Joshua dhidi ya Joseph Parker  utakaofanyika machi 31 huko Cardiff.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni