Mvua zinazoendelea kunyesha zimebomoa nyumba kadhaa huku zingine
zikizingirwa na maji Kata ya Mafisa, Kihonda Manispaa ya Morogoro.
Mvua hizo ambazo bado zinaendelea kunyesha tangu asubuhi zimeziba njia kadhaa mkoani humo na kusababisha mafuriko na kusababisha baadhi ya wanafunzi kushindwa kwenda shule.
Maeneo mengine ya manispaa hiyo yaliyokumbwa na mafuriko hayo ni pamoja na Kichangani, Mazimbu, Chamwino, Mbuyuni, Kilakala, Boma na sabasaba.
Aidha shughuli za biashara kwenye maduka yaliyokuwa katikati ya Manispaa hiyo zilisimama kufuatia maji kuingia kwenye maduka hayo na kusababisha uharibifu wa bidhaa mbalimbali.
Madhara mengine yaliyotokana na mvua hiyo ni kuharibika kwa miundombinu ya barabara kutokana na kujaa maji na hivyo wananchi kulazimika kuvushwa kwa kubebwa mgongoni kwa Sh1000

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni