Chama cha ANC cha Afrika Kusini kimesema hakuna ratiba ya kumwondoa madarakani rais Jacob Zuma kwa sasa.
Chama hicho tawala nchini humo kimeongeza kuwa tayari kimeshajadili
suala la kumwondoa madarakani rais Jacob Zuma wa nchi hiyo, lakini
hakuna ratiba iliyopangwa kufanya hivyo hivi karibuni.Katibu Mkuu wa ANC, Ace Magashule amesema kamati tendaji ya taifa ya chama hicho haijafanya uamuzi wa kumwita na kumhoji rais Zuma, ambaye anashinikizwa kujiuzulu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni