Lau ningekuwa mjinga ningeanza kugombana mm na huyu mchezaji asiyejitambua..kanisukuma bila sababu baada ya game ila nikaona nikichachamaa washabiki wetu wangeweza kumdhuru..uzuri wake niliwaambia Kocha wake Mecky Maxime na nahodha Juma kaseja kabla ya kwenda kumdhuru huyo mshabiki…Nyoso mm sijatoka Buhelelo…Wahangaishe maforeigners mjini….huo undava na uselamavi mm nshavuka huko @official_juma_kaseja #meckymeximeMara baada ya mechi hiyo beki huyo wa Kagera Sugar, Juma Nyoso amejikuta akitiwa mbaroni na Polisi mjini Bukoba kwa madai ya kumtwanga shabiki ngumi mara baada ya mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Kagera Sugar kupigwa 2-0 na Simba SC kwenye dimba la Kaitaba.
Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya mpira kumalizika wachezaji wa Kagera Sugar walikuwa wanakwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo (dressing-room) ambapo inadaiwa kuwa baadhi ya mashabiki wanaoaminika kuwa ni wa Kagera Sugar wakawa wanawarushia maneno makali (matusi) wachezaji hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni