Hali
mbaya ya mafuriko yanayoendela kuathiri wananchi wa Wilaya ya Kilosa
Mkoani Morogoro yamemfanya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Generali
Venance Mabeyo kufika Kilosa na kutembelea baadhi ya maeneo
yaliyoathirika ili kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa kuokoa maisha ya
wananchi wa maeneo hayo na mali zao.
Generali
Mabeyo aliwasili Kilosa Jan.19, 2018 majira ya jioni na kuungana na
mwenyeji wake Dkt. Kebwe Stephen Kebwe Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
aliyepiga kambi Wilayani humo kwa ajili ya mafuriko hayo kisha bila
kujali mvua iliyokuwa inaendelea kunyesha muda wote wakatembelea baadhi
ya maeneo yaliyoakuwa yamethiriwa ili kuona hali halisi ya mafuriko
hayo.
Kwenye
kikao cha majumuisho Mkuu huyo wa Majeshi nchini alishauri kuwa ili
kutatua changamoto hiyo inatakiwa nguvu ya ziada na ya pamoja kwa
taasisi zote kuungana, Ikiwa ni pamoja na taasisi mbali ili kuweza
kuokoa maisha ya watu, mali zao pamoja na miundombinu iliyoathiriwa.
Hata
hivyo alisema changamoto hiyo inatakiwa kuwe na mpango wa muda mfupi,
muda wa kati na muda mrefu. Amesema suluhisho la mpango wa mda mfupi ni
kuwa na kazi ya dharura, na kazi hiyo ya dharura inahitajika kuwepo na
mpango wa dharura ambao ni kuokoa maisha ya watu waliozingirwa na maji
ili wasiendelee kukosa huduma za kijamii na pia kuathiri afya zao kwa
kunywa maji ambayo si salama.
Pamoja
na kuwepo kwa wazo la kurekebisha tuta la mto Mkondoa ikiwa ni mpango
wa muda wa kati ili maji hayo yafuate mkondo wake lakini pia Generali
Mabeyo ameshauri kuangalia namna ya kupunguza kasi ya maji hayo kuanzia
yanakotoka kwa kujenga mabwawa ikiwa ni mpango wa muda mrefu.
“Maji
haya yanakuja huku ni kama sisi ni waathirika zaidi lakini yanakoanzia
hatujui hali iko namna gani, pengine katika mpango wa muda mrefu
ingetazamwa namna ya kuyapunguza haya maji kasi yake.Sasa katika
kuyapunguza, taasisi mablimbali zina wataalamu ambao wanaweza kusaidia
kuweza kujenga mabwawa makubwa huko yanakoanzia ili haya maji kupunguza
kasi yake kabla hayajafika huku” alisema Generali Mabeyo.
Akitoa
maelezo ya awali Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe amesema
tuta hilo la mto Mkondoa lilijengwa enzi za Mkoloni kama kinga kwa mji
wa Kilosa na kwa mara ya kwanza lilipasuka mwaka 2010. Ujenzi wake
kuanzia hapo haukukamilika vizuri kutokan na hali ya kifedha na sasa
limepasuka baada ya Mvua nyingi kunyesha kuamkia Jan,11 mwaka huu.
Hata
hivyo Dkt. Kebwe ametoa Ombi kwa Mkuu huyo wa Majeshi, kupata nguvu
kazi ya wananjeshi, vifaa na utaalamu wao ili baada ya mvua hizi
kupungua waendelee na kutafuta mbinu ya kuuongoza mto Mkondoa uweze
kupita katika sehemu yake ya awali na hivyo kutoathiri wananchi, mali
zao na miundombinu iliyopo eneo hilo .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni