mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Jumamosi, 30 Desemba 2017
Watoto wawili wafa, 126 walazwa kwa kipindupindu
WATOTO wawili wamekufa na wengine 126 wamelazwa katika vyumba vya madarasa vya Shule ya Msingi Nguruka wilayani Uvinza, Kigoma, kutokana na ugonjwa unaodhaniwa kuwa kipindupindu.
Mganga Mkuu wa Kigoma, Dk. Paul Chaote, alisema jana kuwa kituo cha afya cha Nguruka kilipokea watoto 126 Desemba 27, mwaka huu wakikabiliwa na ugonjwa wenye dalili za vimelea vya kipindupindu .
Siku mbili baada ya sikukuu ya Krisimasi watoto 126 wameathirika na vimelea vya wadudu wanaosababisha kuhara na kutapika shida ni usimamizi mbovu wa kanuni za usafi wa mazingira katika uandaaji wa chakula," alisema Dk. Chaote.
Hata hivyo alisema hadi jana walikuwa wamebaki watoto 93 wanaougua ugonjwa wenye dalili za kipindupindu na kwamba leo atatoa tarifa kamili ya majibu ya kina kutoka maabara kwa mujibu wa matokeo ya sampuli ya kipimo cha kinyesi.
Naye Diwani wa Nguruka, Abdallah Masanga, alisema kata hiyo inakabiliwa na matumizi ya visima vifupi na kwamba vingine viko karibu na vyoo.
"Wawili wamekufa na asilimia 80 ya watoto wanaougua ni wa miaka mitano hadi 11. Hakuna mtu mzima na tatizo ni kwamba wananchi hawazingatii usafi kwa kunawa mikono baada ya kutoka chooni na kabla ya kula na msimu wa sikukuu watoto hula ovyo,” alisema.
Alisema jana uongozi wa mkoa na wilaya sambamba na wenyeviti wa vijiji vya kata ya Nguruka, walifanya kikao cha dharura juu ya hatima ya usafi kwa kaya kwa mujibu wa kanuni za afya na kuhamasisha kuwa na vyoo bora na visima vilivyo karibu na choo kufukiwa mara moja ili kuepusha vifo na gharama za tiba kwa ugonjwa wa kipindupindu ambapo jamii ikibadilika hautakuwapo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (mstaafu) Emmanuel Maganga, alikiri shida ya magonjwa ya mlipuko hasa kipindupindu ni utamaduni hasi wa kutokunawa mikono kabla na baada ya kutoka chooni.
"Madiwani mnapopata wafadhili wa mradi wa WASH msihamishie kwenye miradi mingine. Ukweli hatuna utamaduni wa kunawa mikono baada ya kutoka chooni. Hii ni fedheha, Waafrika tubadilike," alisema.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni