
Chura
wa Kihansi kama zilivyo raslimali nyingine ni maliasili muhimu ya
watanzania.Chura wa kihansi aligundulika mwaka 1996 katika mapromoko ya
maji yaitwayo Mhalala yaliyoko ndani ya Milima ya Udzungwa katika Wilaya
ya Kilombero,Mkoa Morogoro.Chura huyu anaishi kwenye mazingira ya maji
yanayotiririka na kutoa mvuke mwingi sana kutokana na nguvu ya
maji.Chura huyu ambae kitalaamu anaitwa Nectophrynoides asperginis
hapatikani sehemu nyingine yeyote duniani isipokuwa katika bonde la
Kihansi nchini Tanzania tu.
Chura wa kihansi ni
chura pekee katika jamii ya vyura waliopo duniani kwa sababu vyura hawa
hutaga mayai na kukaa nayo kwenye kifuko kilichopo ndani ya chura
mwenyewe hadi muda wa kuanguliwa unapofika na ndipo hutoa vitoto hai.Kwa
lugha rahisi ni kwamba Chura hawa huzaa kwa sababu hatagi mayai
yakaonekana bali hukaa ndani ya Chura mwenyewe.
Chura huyu anatofautiana
na vyura wengine kwa sababu vyura wa jamii nyingine hutaga mayai na
kuyaacha majini ambako huanguliwa wakati mama yao hayo,wakati Chura wa
kihansi huangulia tumboni na kuwazaa watoto wakiwa hai,tabia hii ya
kuzaa ndio inayomfanya chura huyu kuwa wa kipekee duniani
Chura huyu amewekwa
kwenye kundi la viumbe wanaolindwa kutokana na kutoweka kwake na kuwekwa
kwenye kifungu cha kwanza cha Mkataba wa Biashara ya Wanyamapori na
Mimea iliyo hatarinikutoweka.Mkataba huu kwa Kiingereza unaitwa
"Convention on International Trade in Endangered Species" (CITES) na
kisheria chura huyu hawezi kufanyiwa biashara ya aina yeyote hapa
duniani.
Maporomoko ya korongo la
Mto Kihansi ambayo ndiyo makazi ya asili ya Chura hawa yana ukubwa wa
eneo la urefu wa Kilometa nne na upana wa nusu Kilometa.Bonde la Mto
Kihansi linapatikana katika mto Kihansi unaoanzia katika Wilaya za
Mufindi na Kilolo Mkoa wa Iringa na kupeleka maji yake katika Wilaya ya
Kilombero Mkoani Morogoro.
Serikali kupitia Wizara
ya Maliasili na Utalii na taasisi zake zimekuwa zikiandaa mradi wa
utunzaji wa mazingira katika bonde la Mto Kihansi "LKEMP" Mradi huu
unasimamiwa na Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira
"NEMC "
Katika kurudisha
mazingira asilia ya vyura hawa,mradi wa "LKEMP"wameweka mabomba
yanayotoa maji yenye uvuke unaofanana na ule wa asilia kwa ajili ya
kurudisha uoto uliokuwapo.Kazi hii imekua ikifanyika kwa kushirikiana na
idara ya Wanyamapori kupitia taasisi yake ya utafiti wa wanyamapori
"TAWIRI" Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira " NEMC" ,Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam na Sokoine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni