Ziwa
Nyasa (katika Malawi: Lake Malawi; katika Msumbiji: Niassa) ni kati ya
maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki ikiwa na nafasi ya tatu baada ya
Viktoria Nyanza na Ziwa Tanganyika.
Lina urefu wa 560 km na upana wa 50-80 km. Vilindi vyake vinaelekea hadi mita 704 chini ya uwiano wa maji yake.
Mwonekano
wa Jiwe la kihistoria kwa ubavuni linalojulikana kwa jina Pomonda
lililopo Ziwa Nyasa lililotumiwa kujificha na wananchi wakati wa Vita
vya Dunia.
Jiwe la POMONDA likionekana kwa nje katika Ziwa Nyasa eneo la Liuli.
Kivutio kimoja
wapo katika Mwambao wa Ziwa Nyasa katika eneo jirani na Jiwe la Pomonda
ni Machweo ya Jua (SUNSITE)kama yanavyoonekana pichani kwa mbali
Jiwe la POMONDA
lililopo katika Ziwa Nyasa hapo ni nje ya Pango ambalo kwa ndani lina
uwezo wa kuhifadhi watu 250 kwa wakati mmoja hapo ni namna maji kupwa
yanavyoonekana pembeni mwa jiwe hilo.
Ufukwe wa Ziwa
Nyasa namna unavyoonekana pichani na kuvutia kwa Madhari ambapo shughuli
za kiuchumi kwa Wananchi wa Ziwa Nyasa huzifanya eneo la Mwambao wa
Ziwa Nyasa au kuvuka Nchi jirani ya Malawi ambayo imetenganishwa na Ziwa
Nyasa.
Washiriki wa
Mdahalo wa Mabadiliko ya HAli ya Hewa uliofanyika Liuli Wilayani Nyasa
kwa Ufadhili wa Foundation for Civil Society wakionyesha Jiwe la POMONDA
linalovutia watalii mbalimbali wanaokuja kutembelea Ziwa Nyasa.
Hapo ni Meli ya
MV Songea ambayo hutumika kusafirisha Abiria na Bidhaa kutoka Tanzania
kuelekea Malawi kupitia Ziwa Nyasa ikiwa imetia Nanga Liuli Ziwa Nyasa
Kutoka eneo la
Ufukwe mpaka kulifikia Pango hili la Pomonda kuna umbali wa kilometa
moja na robo. Pango hili la Pomonda limezungukwa na Miti ya Asili ambayo
uneune wake hauzidi robo mita na umri wa miti hiyo yapata miaka
100,pango hili la Pomonda pia limezungukwa na Mawe yenye umbo la Mafiga
Matatu kuzunguka eneo hilo mpaka kulimaliza unachukua muda wa saa . Hapo
Mwandishi wa Habari Adam Nindi baada ya Kuzunguka katika kulifikia
pango hilo inaonyesha jinsi gani alivyochoka akiwa amelala chini.
Taarifa
zilizotolewa na Wazee waishio katika eneo la Mwambao wa Ziwa nyasa
wamesema kipimo cha ujazo wa Maji ya Ziwa Nyasa kujua yanapungua au
yanaongezeka ni alama hizo zinazoonekana mistari mieupe na rangi nyeusi
kuwa ziwa limepungua maji kwa kiasi kikubwa ambapo awali yalifikia
katika mistari inayoonekana kwenye jiwe hilo
ewa
Kusini mwa ziwa unatoka Mto Shire unaopeleka maji kwenye Mto Zambezi na hatimaye Bahari Hindi.
Kijiolojia ziwa ni sehemu ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.
Eneo
la ziwa ni 29,600 km². Sehemu kubwa ni eneo la Malawi, robo ya
kusini-mashariki ni eneo la Msumbiji, robo ya kaskazini-mashariki ni
eneo la Tanzania. Lakini kuna ugomvi kati ya Malawi na Tanzania kuhusu
mipaka. Malawi imedai ya kwamba maji yote hadi ufukoni upande wa
Tanzania ni sehemu ya eneo lake la kitaifa. Tanzania imedai ya kwamba
mpaka uwepo katikati kufuatana na uzoefu wa kimataifa.
Sababu
ya mzozo ni utaratibu wa kikoloni. Wakati wa Afrika ya Mashariki ya
Kijerumani palikuwa na mpaka wa kimataifa kaskazini mwa ziwa. Baada ya
1919 Uingereza ilitawala Tanganyika pamoja na Malawi (Nyasaland). Kwa
kusudi la kurahisisha utawala mambo yote yaliyohusu ziwa yaliwekwa chini
ya serikali ya kikoloni ya Nyasaland. Baada ya uhuru Malawi ilijaribu
kutumia uzoefu huo kama haki yake ya kitaifa. Polisi yake ilijaribu
kutawala wavuvi na feri za Tanzania ziwani. Mzozo huu ulisababisha
risasi kufyatuliwa baada ya uhuru. Hadi leo hakuna mapatano rasmi lakini
nchi zote mbili zinaendelea bila kutumia nguvu. Hali halisi Malawi
imeheshimu dai la Tanzania halikusumbua tena wavuvu au feri za jirani
ndani ya robo ya kaskazini-mashariki ya ziwa.
Ziwa
Nyasa linajulikana kuwa na aina nyingi za samaki (zaidi ya 1500). Aina
chache tu zinavuliwa kama chakula lakini aina mbalimbali zinakamatwa na
kuuzwa nje ya Afrika kwa wapenzi wa samaki zenye rangi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni