
Wabunge
wa Chadema, Joshua Nassari (Arumeru Mashariki), Godbless Lema ( Arusha
Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa(Iringa Mjini) wamewasilisha Takukuru
ushahidi wanaodai unaonyesha jinsi madiwani wao walivyonunuliwa kwa
kupewa rushwa.
Wabunge
wao, wamewasilisha ushahidi huo mchana wa leo Jumatatu kwenye ofisi za
Makao Makuu ya Takukuru zilizopo Upanga Dar es Salaam.
Wabunge hao wamewasili katika ofisi hizo saa 8.39 mchana na kukutana na waandishi wa habari waliokuwa wakiwasubiri.
Katika
kile ambacho waandishi hawakukifikiria, wabunge hao waliwasili kwa
miguu na kuelekea moja kwa moja ndani ambapo waandishi walizuiwa
kuingia.
Ushahidi
huo, wameuwasilisha ikiwa imepita siku moja tangu Lema na Nassari
walipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha kueleza jinsi
madiwani wao walivyoshawishiwa na kwa rushwa kuihama Chadema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni