Baada ya duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika
kwa timu 16 kushuka katika viwanja mbali mbali kuzisaka pointi tatu
muhimu mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2000 klabu ya Mtibwa Sugar inashika
msukani katika msimamo kwakuwa na alama 10.
Katika msimamo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Klabu Bingwa ya
Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeendelea kufanya vizuri nakushika
nafasi ya pili baada ya hapo jana Usiku kuifunga Lipuli FC.
Klabu ya Singida United ambayo imepanda msimu huu ikiwa chini ya
Mwalimu Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm inashika nafasi ya
tatu na kuwazidi wakongwe klabu za Simba SC inayoshika nafasi ya nne na
Young Africans inashika nafasi ya sita.
Chati nzima ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni