Jumatatu, 2 Oktoba 2017

Asilimia 90 wakubali Catalonia kujitenga na Uhispania, Mahakama yatoa tamko

Asilimia 90 ya kura zilizopigwa Jumapili hii huko Uhispania katika eneo la Catalonia, zimetaka eneo hilo kujitenga na nchi hiyo.



Hata hivyo Mahakama ya katiba nchini humo imedai kuwa, kura hizo zilikuwa kinyume na sheria. Kwa mujibu wa shirika la habari la CNN watu takribani 844 walijeruhiwa katika maandamano yaliyotokea kati ya wananchi wa eneo la Catalonia na polisi.Kiongozi wa eneo la Catalonia, Carles Puigdemont aliyeshika ua la rangi nyekundu
Kiongozi wa eneo hilo, Carles Puigdemont amesema kura hizo zimewapa haki watu wa eneo hilo baada ya mateso ya muda mrefu. “Leo, siku hii yamatumaini na mateso pia, wananchi wa catalonia wameshinda haki ya kujitegemea kama taifa huru,” amesema kiongozi huyo.”
Hizi ni picha za matukio mbalimbali yaliyotokea katika uchaguzi huo.




 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni