Jumanne, 19 Septemba 2017

Sababu ya wachezaji wa Yanga kugomea mazoezi leo



 Baada ya uongozi wa Yanga kusema wachezaji wake walikuwa wamepanga kutofanya mazoezi leo, taarifa zinaeleza kuwa ni kweli waligoma.

Wachezaji wa Yanga, waligoma kufanya mazoezi leo asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na baadaye uongozi wa Yanga ukasema ilikuwa ni programu ya mwalimu.

Lakini habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinaeleza waligoma kwa kuwa hawajalipwa mishahara yao ya miezi miwili.

“Kweli ni mishahara ya miezi miwili, hii ndiyo imesababisha tusifanye mazoezi,” kilieleza chanzo cha uhakika.

“Unajua uongozi umekuwa ukitoa ahadi lakini unashindwa kutekeleza na sasa wachezaji mambo yamekuwa magumu.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni