Jumapili, 17 Septemba 2017

DC Monduli kathibitisha linalodhaniwa bomu kuuwa watoto watatu




Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Idd Kimanta amethibitisha kuwa watoto wawili wamefariki baada ya kulipukiwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu wakati wanachunga mifugo yao kwenye eneo la Jeshi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ ambalo hufanyia mazoezi.
DC Kimanta amesema tukio hilo limetokea Ijumaa jioni katika Kijiji cha Nafco kilichopo katika Kata ya Loksale Wilayani Monduli katika eneo linalotumiwa na Wanajeshi kwa ajili ya kufanyia mazoezi na hakuna mtu anayeruhusiwi kufanya shughuli yoyote katika eneo hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni